Jennifer Kumwembe: Niliuza Baga

“Niliondoka  nchini kwenda Marekani, mwaka 1999 na mwaka 2007 nilirejea nyumbani kwa mara ya kwanza. Katika maongezi na familia yangu na jamii jinsi walivyopata taabu kupata huduma za afya, nikaumua moyoni, ndipo nikaweka lengo la kuanzisha Zahanati ya Cignat,”anasema Jennifer.HAKIKA “mwenda kwao si mtumwa” na jambo lolote jema huanzia nyumbani. Kauli hizo zinakamilishwa kwa vitendo na Jennifer Salome Kumwembe.
Jennifer ni Mtanzania anayeishi Marekani, lakini kwa kutambua umuhimu wa nyumbani, amerudi kuwekeza nchini kwa kufungua zahanati na kutoa ajira kwa wanawake wengine 12.
“Niliondoka  nchini kwenda Marekani, mwaka 1999 na mwaka 2007 nilirejea nyumbani kwa mara ya kwanza. Katika maongezi na familia yangu na jamii jinsi walivyopata taabu kupata huduma za afya, nikaumua moyoni, ndipo nikaweka lengo la kuanzisha Zahanati ya Cignat,”anasema Jennifer.